Funguo Saba za Kuyashinda Yasiyowezekana
Funguo Saba za Kuyashinda Yasiyowezekana ni kitabu kinachoelezea namna matarajio makubwa ya mafanikio yanavyoweza kuhafifishwa na imani ya kawaida. Ili kupata matokeo makubwa na ya kushangaza, yakupasa kubadili namna ya kutenda na kumwamini Mungu. Ukiwa na imani thabiti yenye matarajio makubwa kwa Mungu hutafanya mambo ya kawaida na kwa mazoea. Dhambi imeleta mauti na pia dhambi imemtenga Mungu na wanadamu.
Ukidumu katika misingi ya kumtumaini Mungu siku zote; jambo hili litakufanya usiyachukulie maagizo ya Mungu kuwa ni mazoea na ya kawaida. Mabadiliko thabiti ya nafsi, mwili na roho yatadhihirika pindi Yesu Kristo atakapokuwa ndani ya maisha yako. Hakuna litakaloshindikana kwako kamwe!
Yaliyomo
➡ Dibaji … 4
➡ Shukrani … 5
➡ Maelezo Muhimu … 6
➡ Sura ya 1: Umetangaza Vita … 7
➡ Sura ya 2: Ufunguo wa Kwanza … 19
➡ Sura ya 3: Ufunguo wa Pili … 24
➡ Sura ya 4: Ufunguo wa Tatu … 30
➡ Sura ya 5: Ufunguo wa Nne … 38
➡ Sura ya 6: Ufunguo wa Tano … 44
➡ Sura ya 7: Ufunguo wa Sita … 72
➡ Sura ya 8: Ufunguo wa Saba … 81
➡ Sura ya 9: Mwitikio Wetu … 87
Onyo
Haki Zote Zimehifadhiwa. Huruhusiwi kutoa nakala ya kitabu hiki au sehemu ya kitabu hiki kwa sababu yoyote ile bila ruhusa ya mmliki wa kitabu kwa maandishi. Juhudi zimetumika kuandaa kitabu hiki kwa usahihi na umakini mkubwa sana kwa lengo la kutoa elimu na ujumbe ulio bora zaidi.
Ikithibitika kwa namna moja au nyingine umehusika kudurufu nakala au kusambaza katika mitandao ya kijamii na mingieyo nakala ya kitabu hiki utakuwa umetenda uharifu chini ya sheria ya makosa ya mtandao. Adhabu ya kifungu au faini au vyote kwa pamoja vinaweza kutolewa dhidi yako. Epuka wizi, kuwa mzalendo kwa kununua kazi za wasanii wetu. Wizi haukubaliki kiimani na hata kijamii.
Hata hivyo, taarifa, ujumbe au mafunzo yanayopatikana katika kitabu hiki hayana uhusiano wowote na matokeo ya msomaji. Mwandishi, mchapishaji au msambazaji hatawajibika kwa tatizo lolote litakalojitokeza kutokana na usomaji wa kitabu hiki.
Juliana –
Napenda sana vitabu vyako, Mungu akubariki